Karibu kwenye tovuti ya Kanisa la Waadventista

Mbeya Kati


TAMKO LA UTUME 

UTUME WETU:

Utume wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mbeya Kati, ni kuwafanya watu wote wawe wanafunzi kwa kuwapelekea Injili ya milele iliyo katika muktadha wa Ujumbe wa Malaika Watatu wa Ufunuo 14:6-12, kuwaongoza wampokee Yesu kama Mwokozi wao binafsi, na kuwaita kujiunga katika Kanisa lake la Masalio, wakifundishwa kumtumikia Yeye kama Bwana wao na kuwaandaa kwa Marejeo yake yaliyo karibu.

UTEKELEZAJI WA UTUME WETU:

Tunatekeleza Utume wetu chini ya uongozi na uwezeshaji wa  Roho Mtakatifu kwa kufanya yafuatayo:

  • Kuhubiri – Kwa kulikubali agizo la Kristo la Mathayo 28:18-20, katika siku hizi za mwisho, tunautangazia Ulimwengu wote Injili ya Milele ya Upendo wa  Mungu, anayefunuliwa wazi kupitia maisha , utume, kifo, ufufuo na huduma ya ukuhani wa mwanaye Yesu Kristo.  Kwa kutambua kwamba Biblia ni kitabu cha Mungu kisichoweza kukosolewa, kinachofunua mapenzi ya Mungu, tunaueleza ukweli wote wa Biblia, ukiwemo ule wa kuja kwa Kristo mara ya pili na mamlaka endelevu ya Amri Kumi za Mungu, zenye ujumbe wa kutukumbusha kuitakasa siku ya saba ya juma kama Sabato.
  • Kufundisha – Tukikiri kwamba maendeleo ya mwili na tabia ni vya muhimu katika mpango wa Mungu wa Ukombozi, tunahimiza ukuaji katika kumwelewa Mungu na jinsi ya kuhusiana na Yeye, na Neno lake, pamoja na vitu vyote alivyoviumba.
  • Uponyaji – Kwa kuzithibitisha kanuni za  Biblia za kuwa na utu wote mkamilifu, tunafanya utunzaji wa afya zetu na uponyaji wa wagonjwa kuwa kipaumbele chetu.  Kwa kuwahudumia maskini na wanaoteseka, tunashirikiana na Muumba katika kazi yake ya urejeshwaji kwa njia ya matendo ya huruma.
  • Kufanya wanafunzi Kwa kuthibitisha ukuaji wa kiroho ulio endelevu kwa maendeleo ya waumini, tunatoa malezi kwa waumini wapya, tukiwafunza kuishi maisha ya haki na kuwaelekeza kushuhudia kwa mguso wenye nguvu na kuwatia shime kuonyesha mwitikio wa utii kwa mapenzi ya Mungu.

NJOZI YA UTUME WETU:

Kwa kupatana na unabii unavyofunuliwa katika Maandiko, tunauona utume wetu ukifikia kilele katika Mpango wa Mungu wa urejeshwaji wa viumbe vyake katika ukamilifu wa mapenzi yake na haki yake.

 

MAAFISA NA WAKURUGENZI WA NYANDA ZA JUU KUSINI

Southern Highlands Conference Officers 2010 - 2015

President: Pr. Joseph Mngwabi

Executive Secretary: Pr Elias Lomay

Treasurer: Mr. Douglas K Mwambeta

DEPARTMENTAL DIRECTORS

Personal Ministries, Ministerial Association, Family Life & Global Mission:

Pr. Filbert Mwanga

Stewardship, Development & Trust Services:

Pr.Kennan Mwasomola

Education, Religious Affairs:

Mr. Abraham Youze

Women, Children Ministries & Sabbath School:

Mrs. Hodiah Mutani

Publishing& School of Prophecy:

Pr. Ezekiah Chaboma

Youth, Chaplaincy & Public Relations:

Pr. Deogratius R. Bambaganya

Health Ministries & HIV AIDS Coordinator:

Pr. Makaki M. Biseko

Communication, IT, AWR, VOP  & Satellite:

Pr. Haruni N. E Kikiwa